Wakazi wa Ng’ambi wametakiwa kupanda miti ili kuepuka mafuriko
31 March 2021, 11:06 am
Na; Selemani Kodima.
Wakazi wa kata ya Ng’ambi wilayani Mpwapwa wametakiwa kuhakikisha wanapanda miti pembezoni mwa vyanzo vya maji ikiwemo Mito ya maji ili kuzuia Mafuriko yanayotokea wakati wa Msimu Mvua za Masika.
Wito huo umetolewa na Diwani wa Kata ya Ng’ambi Bw Richar D Milimo alipo kuwa akizungumza na Taswira ya Habari kuhusu Jitahada ambazo wameendelea kuzichukua Baada ya kuanza Zoezi la Ujenzi wa Daraja la Ng’ambi ambalo lilibomolewa na Mafuriko yaliyosababishwa na Mvua za Masika.
Bw Malimo amesema wameamua kuchukua hatua ya kupanda miti katika Vijiji vya Ng’ambi,Kiegea ,Mbugani na Kazania ili kusaidia Kurejesha Uoto wa Asili katika Mto ulio pita katika vijiji hivyo.
Amesema kukosekana kwa Miti ya kutosha katika eneo ambalo daraja la Ng’ambi linapatikana ni mojawapo ya sababu inayosababisha uwepo wa mafuriko makubwa katika eneo hilo msimu wa mvua .
Pamoja na hayo amesema wananchi wameitikia wito wa kuotesha miti katika eneo hilo hali inayo leta Faraja ya kukijanisha kata ya ng’ambi na maeneo ya mto huo.