Vijana Bahi wapigwa marufuku kucheza pool table muda wa kazi
16 June 2023, 12:43 pm
Yeyote atakayekutwa anacheza pool table muda wa kazi hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake na atachukuliwa kama mzurulaji na atashtakiwa kisheria.
Na Bernad Magawa.
Jeshi la polisi wilayani Bahi limepiga marufuku vijana kucheza pool table muda wa kazi na kusema kuwa wale wote watakaokaidi agizo hilo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Akizungumza na baadhi ya vijana wa kijiji cha Msisi wilayani humo ambao walikutwa wakicheza mchezo huo muda wa kazi, kamanda wa Jeshi la Polisi wilaya ya Bahi SSP Idd Ibrahim amekemea vikali kitendo hicho na kusema wote watakaokutwa wakicheza mchezo huo wakati wakazi watachukuliwa kama wazurulaji na watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Kamanda Ibrahim amewaasa vijana kutumia muda wao vizuri kwa kufanya kazi za kujiongezea kipato badala ya kukaa mitaani wakicheza michezo ambayo haina faida katika maisha yao ya badae.
Aidha ameelekeza muda sahihi ambao vijana wanaweza kucheza mchezo huo na kuwaagiza wamiliki wa michezo hiyo kuheshimu kanuni na taratibu za nchi.