SUMA JKT yazindua mitambo mikubwa ya kuzalisha na kusafirisha zege
25 May 2023, 4:37 pm
Amewaagiza watendaji wa SUMA JKT kuhakikisha wanasimamia mitambo hiyo ili ilete tija iliyokusudiwa katika kuongeza ufanisi wa SUMA JKT.
Na Alfred Bulahya.
Jeshi la Kujenga Taifa kupitia SUMMA JKT, limezindua rasmi mitambo mikubwa ya kuzalisha na kusafirisha zege yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.349 za kitanzania itakayokuwa ikitumiwa kuzalisha zege.
Akizungumza katika eneo la Kisasa jijini Dodoma mara baada ya kuzindua mitambo hiyo Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema kuwa uzinduzi wa mtambo huo unakwenda kuiwezesha SUMA JKT, kuondokana na gharama kubwa walizokuwa wakitumia kununua zege, kukodi magari na kuzisafirisha kwenye miradi yake mbalimbali.
Aidha amewaagiza watendaji wa SUMA JKT kuhakikisha wanasimamia mitambo hiyo ili ilete tija iliyokusudiwa katika kuongeza ufanisi wa SUMAJKT.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Ujenzi SUMA JKT, Mhandisi Morgan Nyoni,amesema mitambo hiyo imeingizwa nchini Januari 16, 2023 na kumaliza kusimikwa May 22, 2023 jijini Dodoma.