Utupaji taka ovyo unavyo haribu mazingira
5 August 2024, 5:05 pm
Wananchi wanapaswa kuendelea kutunza mazingira kwa kutotupa taka ovyo, kupanda miti ili kuifanya dunia kuwa mahali salama pa kuishi.
Na Mariam Kasawa.
Utupaji wa taka ovyo unatajwa kuharibu mazingira kwa kiasi kikubwa kwa kusababisha taka nyingi kusambaa ovyo.
Jiji ya Dodoma inakisiwa kuzalisha tani 350 za taka ngumu kwa siku ambapo kata za nje ya mji uzalishaji tani 114 na Kata za mjini uzalisha ni tani 236. Aidha wastani wa tani 150 tu ndiyo zinaondoshwa mjini kwa siku sawa na asilimia 66%, hali hiyo imekuwa ikichangiwa na uhaba mkubwa wa vifaa hasa Skip bucket kwani kwa sasa zipo 61 kati ya 187 zinazohitajika kwa sasa kwa mujibu wa mwongozo.
Uzoaji wa taka katika maeneo mbalimbali ya mji, vikundi vya kijamii vimekuwa vinatoa huduma ya kuzoa taka katika ngazi ya kaya, na maeneo mbalimbali ya biashara na kupeleka katika vituo vya kupokelea taka (collection point) ambapo kuna makasha ya kupokelea taka (Skip buckets). Halmashauri inasafirisha taka mpaka kwenye dampo la kisasa lililoko eneo la Chidaya Kata ya Matumbulu.
Dampo la Kisasa la Chidaya lina Ukubwa wa Hekari 48 ambapo eneo linalotumika kwa sasa lina Ukubwa wa Hekari 10. Dampo hili lina uwezo wa kutumika kwa muda wa miaka 18 hadi 20.
Dampo hili linapokea taka kila siku kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 12 jioni. Taka hupimwa katika mizani iliyopo katika geti la kuingilia dampo ili kujua uzito wake kwa kila gari inayoleta taka Dampo na kutunza takwimu.
Wastani wa tani 120 -150 za taka ngumu hutupwa katika Dampo kila siku kutoka katika vyanzo mbalimbali vya uzalishaji taka.
Kwa mujibu wa UN-HABITAT wanasema kwamba taka zinaweza kuleta madhara makubwa kwa afya ya umma, mazingira na hali ya hewa, lakini katika zama hizi sayansi, teknolojia na ubunifu wa hali ya juu vinaweza kuleta suluhu ya gharama nafuu katika changamoto hiyo ya taka na kuisaidia miji na jamii kuziona taka kama ni fursa ya biashara.
Siku ya UN-Habitat duniani: Ikumbukwe kuwa Siku ya Makazi Duniani, (UN-HABITAT )iliwekwa na Umoja wa Mataifa kufanyika kila Jumatatu ya kwanza ya Mwezi Oktoba ambapo Siku hiyo iliwekwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa azimio 40/202 na kuadhishwa kwa mara ya kwanza kunako mwaka 1986. Lengo ni kutaka kutafakari juu ya Makazi yetu katika miji, juu ya haki ya kuishi katika makazi salama .