Dodoma FM

Mifuko ya plastiki tishio kwa Afya za walaji

1 August 2024, 4:03 pm

Picha ni mama lishe kutoka soko la miembeni akiongea na Dodoma tv .Picha na Mariam Kasawa.

Dkt. Harrison anaeleza kuwa kwa Afrika, plastiki zinazozalishwa au kuingizwa barani, zikipata joto zinatoa vipande vidogo vya plastiki vyenye sumu.

Na Mariam Kasawa.
Mifuko ya plastiki inathibitika kisayansi ni hatari kwa mazingira na afya ya binadamu na viumbe wengine.

Baadhi ya mama na baba lishe wanaonekana kutokuwa na uelewa na matumizi ya plastiki kwani mara nyingi wanatumia mifuko ya plastiki kuhifadhi chakula ili kibaki kuwa chamoto .

Hali hii inanifanya kufika katika soko la Miembeni ambalo lina akina mama na baba lishe wengi kutaka kufahamu kama wanatambua madhara ya kuhifadhi chakula chamoto kwenye mifuko ya plastiki ambapo wamedai kuwa hawafahamu madhara yeyote na mbinu hii wanaitumia kwa muda mrefu.

Sauti za baba na mama lishe.

Nafika kwenye mgahawa wa mama Chai hapa soko la Miembeni yeye anasema mbinu ya kuhifadhi chakula kwenye mifuko ya plastiki ni hatari na limepitwa na wakati hivyo anawataka mama lishe wenzake kubadilika na kutumia mbinu zingine ambazo hazihatarishi afya za walaji.

Picha ni Bi Luvilo Mwamilo kaimu meneja wa utekelezaji wa sheria kutoka NEMC.Picha na NEMC.
Sauti ya mama lishe.

Kwa mujibu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC, tani 350,000 za mifuko ya plastiki huzalishwa kila mwaka.

Bi Luvilo Mwamilo kaimu meneja wa utekelezaji wa sheria kutoka NEMC anaendelea kuwaeleza wananchi juu ya katazo la mifuko ya plastiki na madhara yake.

Sauti ya Bi.Luvilo Mwamilo .

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam, Harrison Chuwa, anasema kuna uwezekano wa kupata saratani kutokana na matumizi ya mifuko ya plastiki katika kupika na kuhifadhi chakula.