Dodoma FM

Recent posts

30 March 2021, 12:15 pm

Dkt.Mpango apitishwa kuwa makamu wa rais bila kupingwa

Na,Mindi Joseph. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan amemteua Dk.Phillipo Mpango aliyekuwa waziri wa Fedha na Mipango  kuwa makamu wa Rais na kupitishwa na Bunge kwa asilimia 100. Jina la Mpango limesomwa Bungeni jijini Dodoma leo…

30 March 2021, 11:43 am

Shughuli ndogondogo ni chachu ya kujikwamua kwa walemavu

Na; Thadey Tesha Wito umetolewa kwa watu wenye ulemavu jijini hapa kujishughulisha na kazi mbalimbali zilizopo ndani ya uwezo wao ili kupunguza utegemezi katika jamii. Wito huo umetolewa na baadhi ya viongozi wa karakana ya watu wenye ulemavu Mkoani Dodoma…

30 March 2021, 8:54 am

Philip Mpango athibitishwa kuwa Makamu wa Rais Tanzania

Na; Mariam Kasawa RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kupitia kwa mpambe wake, leo Machi 30, amewasilisha Bungeni jina la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. . Jina hilo liliwasilishwa bungeni asubuhi ya leo Jumanne machi 30…

29 March 2021, 11:19 am

Idilo , Mpwapwa walia na ukosefu wa huduma ya Afya

Na,Mindi Joseph Wakazi wa kijiji cha Kisokwe wilayani Mpwapwa wapo mbioni kuepukana na adha ya kukosa huduma ya Afya kijijini hapo kutokana na ujenzi wa kituo cha Afya kukaribia kukamilika. Akizungumza na Dodoma Fm Diwani wa kata ya Mazae Mwl.…

29 March 2021, 10:02 am

Taasisi zatakiwa kuongeza ubunifu ili kuleta mageuzi sekta ya kilimo

Na; Rabiamen Shoo. WAZIRI wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda amezitaka Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo, kuongeza ubunifu ili kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo sambamba na kuchochea ukuaji wa sekta ya viwanda na kilimo nchini. Akizungumza baada ya kuzindua…

29 March 2021, 6:00 am

Ripoti ya CAG yabaini madudu hati 98

Na; Mariam Kasawa. Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kicheere imeendelea kubaini dosari ya matumizi ya fedha yanayofanywa na Taasisi na Mashirika ya umma pamoja na vyama vya siasa. CAG amesema kati ya hati…

29 March 2021, 5:55 am

CAG, TAKUKURU Zaagizwa kufanya uchunguzi BOT

Na; Mariam Kasawa. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kushirikiana kwa pamoja kuchunguza fedha zilizotoka Benki kuu ya Tanzania kwa kipindi cha Januari…

26 March 2021, 11:52 am

Magufuli atakumbukwa kwa utendaji wake

Na; Mariam Kasawa. Hayati Dkt.John Pombe Magufuli atakumbukwa kwa  utendaji kazi wake kwani alikuwa hodari tangu akiwa Waziri hadi  alipoteuliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hayo yamesemwa na Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete…

26 March 2021, 11:23 am

Vyombo vya ulinzi na usalama vitamtii Rais Samia

Na; Mariam Kasawa Mkuu wa Majeshi  nchini Tanzania (CDF) Venance Mabeyo amemuhakikishia Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vitamtii na kutekeleza majukumu yake kama ilivyoainishwa kwenye Katiba ya Jamhuri…

26 March 2021, 10:29 am

Wakazi wa Chamwino waahidi kuziishi ndoto za Rais Magufuli

Na Selemani Kodima Mkuu wa wilaya ya Chamwino Vumilia Nyamoga amesema wataendelea kumkumbuka Hayati Magufuli kwa Juhudi zake ambazo alizionesha kwa wakazi wa Chamwino katika Huduma za Msingi ikiwemo Huduma ya Maji na umeme. Bi Nyamoga amesema Hayati Magufuli alionyesha…