Viongozi wa dini watakiwa kupinga vitendo vya ukatili
3 December 2024, 12:08 pm
Kwa mujibu wa Ofisi ya maendeleo ya jamii Mkoani Dodoma kuanzia Januari hadi Agosti mwaka 2024 matukio ya ukatili yaliyoripotiwa mkoani Dodoma ni 2,352, ambapo ukatili kwa watoto ni 629 huku watu wazima ni matukio 1,723 (wanaume 350 na wanawake 1,373).
Na Yussuph Ally.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Alhaj Jabir Shekimweri, amewataka viongozi wa dini kuwa mstari wa mbele kupinga na kukemea vitendo ya ukatili.
Wito huo umetolewa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ushirika wa Akiba na Mikopo isiyo na Riba (TAMPRO SACCOS) Tawi la Dodoma, iliyofanyika Jijini Dodoma.
Alhaj Shekimweri amesema ukatili wa kijinsia na unyanyasaji vinapaswa kushughulikiwa kwa bidii, akisisitiza umuhimu wa kuchukua hatua kuanzia ngazi ya familia.
Miongoni mwa makundi ambayo yanaathirika na ukatili ni pamoja na watu wenye wenye ulemavu kama ambavyo anabainisha Bi. Rukia Ahmed Kassim ambaye ni mlemavu wa macho na ni mtumishi wa Hospital ya Rufaa ya Dodoma anayehudumu kama mfamasia.