Ukosefu wa elimu ya jinsia unavyochangia maambukizi ya vvu kwa vijana
1 December 2020, 6:54 am
Na,Mariam Matundu
Dodoma.
Ukosefu wa elimu ya jinsia kwa vijana kuanzia ngazi ya familia inatajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazopelekea takUwimu za maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa vijana kuwa juu kuliko kundi lolote.
Akizungumza na Taswira ya habari mtaalamu wa afya ya uzazi kutoka chama cha uzazi na malezi bora Tanzania UMATI Godlove Isdoriy amesema kumekuwa na changamoto ya vijana kupata elimu sahihi kuhusu masuala ya uzazi na virusi vya Ukimwi hali inayochochea maambukizi .
Naye Catherine Fredric kutoka kituo amani haki na msaada wa kisheria amesema wanatoa msaada wa kisheria kwa wanaonyanyaswa kwa kulazimishwa kufanya vitendo ambavyo vinahatarisha afya zao.
Tarehe mosi Desemba kila mwaka huadhimishwa siku ya Ukimwi duniani ambapo kwa Mkoa wa Dodoma yatafanyika katika viwanja vya Nyerere ambapo elimu ya vvu,uzazi wa mpango,matumizi sahihi ya kondom vitatolewa .