Jamii imetakiwa kuzingatia fursa za uchumi nchini na kufanya kazi kwa bidii
18 October 2021, 11:18 am
Na; Shani Nicolous.
Jamii imetakiwa kuzingatia fursa za kiuchumi nchini na kufanya kazi kwa bidii ili kutokomeza umaskini nchini.
Akizungumza na Taswira ya habari mchambuzi wa masuala ya kiuchumi na mkuu wa fedha katika Chuo kikuu cha mtakatifu Yohana Dodoma (st John) amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa kuchangamkia fursa na kuongeza juhudi ya kazi ili kutokomeza umasikini.
Amesema kuwa elimu ni msingi mkubwa wa kumtoa mtu katika hali duni kimaisha hivyo kuna haja ya kuwa na mitaala yenye kutengeneza vipaji na ubunifu kwa watu baada ya masomo kuliko kusubiri kuajiriwa.
Kwa upande wake mtafiti wa magonjwa ya kuambukiza kutoka {COHASO} Calvin Swai amesema kuwa hakuna mafanikio kwa mtu asiekuwa na afya njema kwa hali hiyo kuna kila sababu kuzingatia afya na kufuata maelekezo yanayotolewa na mamlaka za afya ili kuepusha umaskini unaotokana na afya duni za watu fulani.
Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya wananchi jijini hapa ambao wamezungumza kuwa vijana ni tegemezi nchini hivyo waache kufanya kazi kwa mazoea na kuridhika na kipato kidogo
Oktoba 17 jana ilikuwa ni siku ya kutokomeza umaskini duniani, ambalo ni lengo la kwanza la malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa SDGS ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaja mambo matatu yanayopaswa kufanyika ili kutokomeza umaskini miogoni mwayo ni kuondoa hewa chafuzi na kutokuzalisha kabisa hewa za ukaa,