Serikali yaombwa kutoa elimu dhidi ya vitendo vya ukatili wa jinsia kwa jamii
19 August 2021, 1:21 pm
Na; Benard Filbert.
Baadhi ya wakazi Jijini Dodoma wameiomba Serikali kuhakikisha wanatoa elimu katika jamii kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia na ubakaji ili kusaidia kukomesha tatizo hilo.
Wamesema hayo wakati wakizungumza na taswira ya habari wakati wakielezea nini kifanyike ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo vimekuwa na athari kubwa katika jamii.
Sayayi Abdala pamoja na William Lukayo ni wakazi wa Jiji la Dodoma wameiambia taswira ya habari kuwa jamii haina uelewa wakutosha kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia pamoja na ubakaji hivyo mamlaka husika ikiwepo dawati la jinsia wanatakiwa kutoa elimu hali itakayosaidia kukomesha vitendo hivyo.
Jerda Luyangi ni ni mkaguzi msaidizi wa polisi kitengo cha dawati la jinsia Wilaya ya Dodoma amesema ili kukomesha vitendo hivyo ni lazima elimu itolewe vyakutosha kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwepo vyombo vya habari ili kila mmoja awe na uelewa.
Hata hivyo amesema kila kata inawasaidizi wa dawati la jinsia lengo ikiwa ni kukabliana na ukatili wa kijinsia pamoja na ubakaji.
Jamii inasisitizwa kutokufumbia macho suala la ukatili wa kijinsia na badala yake kutoa taarifa katika vyombo husika pale wanapoona viashiria vya ukatili wa kijinsia.