Uhamasishaji mdogo wapelekea watu wenye ulemavu kuto nufaika na mikopo ya halmashauri
2 July 2021, 11:19 am
Na; Mariam Matundu.
Imeelezwa kuwa kukosekana kwa taarifa na uhamasishaji kwa watu wenye ulemavu kujiunga katika vikundi ni moja ya sababu inayo pelekea kundi hilo kutopata mikopo kwa wingi inayotolewa na halmashauri.
Hayo yamesemwa namwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wilaya ya Kondoa bwana Abedi Dutu ambapo amesema uhamasishaji kwa watu wenye ulemavu wanaoishi maeneo ya vijijini kuomba mikopo upo chini hivyo wengi wao hukosa fursa hiyo.
Taswira ya habari imezungumza na Bwana Juma Iyulu ambae ni miomgoni mwa watu wenye ulemavu walionufaika na mikopo hiyo wilayani hapo amesema mkopo alioupata licha ya kuendeleza biashara yakeya kuuza matunda pia umemsaidia kuboresha nyumba anayoishi.
Pamoja na watu wengine kunufaika lakini katika kijiji cha Loo kilichopo pembezoni mwa wilaya hiyo bado kuna kundi kubwa la watu wenye ulemavu walioshindwa kupata mikopo hiyo kutokana na changamotio mbalimbali ikiwemo mrorongo mrefu wa kukamilisha taratibu za kusajiri vikundi .
Akijibu baadhi ya malalamiko ya watu wenye ulemavu, Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa kondoa bwana Msoleni Dakawa amesema lengo la kutaka barua za maombi ya mkopo kupitishwa katika ngazi mbalimbali ni kwa ajili ya kupata taarifa sahihi na kuwataka viongozi wa serikali za mitaa kuwasaidia watu wenye ulemavu kurahisisha utaratibu huo.
Halmashauri ya mji wa kondoa imeshakopesha vikundi vitano vya watu wenye ulemavu kutoka mwaka 2018 hadi mwaka huu 2021.