Watanzania wametakiwa kuwa na imani na chanjo ya Corona
18 May 2021, 12:49 pm
Na; Yussuph Hans
Wananchi wametakiwa kuwa na imani na chanjo ya covid 19
Akizungmza na Dodoma fm mtaalamu wa uchunguzi tiba kitengo cha maabara kutoka hospitali ya KCMC Dkt.Ahmed Zubeir amesema kuwa katika matumizi ya tiba wakati mwingine huwa na matokeo hasi hali inayosababisha sintofahamu kwa mtumiaji.
Ameongeza kuwa chanjo ya corona ni vyema wananchi wakawa na imani nayo, kwani suala hilo limepitia hatua mbalimbali katika mikono ya wataalamu na kuona namna ya kutoa chanjo hiyo pasipo kuwepo na athari.
Kuhusu suala la tiba mbadala Dkt.Ahmed amesema kuwa tiba hizo ni bora, lakini ni muhimu kuwepo na chanjo kwani yenyewe itasaidia kukinga na kusambaa kwa ugonjwa huo ambao unabadilika katika hatua mbalimbali.
Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya wananchi jijini Dodoma kuhusu chanjo ya korona nchini, ambapo wamebainisha kuwa na hofu kutokana na matokeo hasi pamoja na wakielezea kufahamu athari za kusambaa kwa ugonjwa huo.
Hapo jana Kamati ya kitaalamu iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan kufanya tathmini ya hali ya ugonjwa wa corona nchini, imetoa mapendekezo 19 ikiwamo matumizi huru ya chanjo ya ugonjwa huo, ili kutoa fursa ya kinga kwa makundi maalumu kama wazee, wenye magonjwa sugu na wahudumu wa afya.