Imani ndogo usimamizi wa fedha changamoto kwa wanawake
17 May 2021, 1:40 pm
Na; Yussuph Hans
Ujuzi wa usimamizi wa masuala ya fedha pamoja na kukosa umiliki wa uchumi ni baadhi ya changamoto ambazo zimeendelea kuwakumba Wanawake Nchini.
Licha ya changamoto hizo kumekuwepo na kundi la wanawake ambao wanamiliki Uchumi kupitia Ajira katika sekta mbalimbali huku wakikumbana na changamoto ya Mazingira wezeshi katika maeneo yao ya Kazi.
Akizungumza na Taswira ya Habari Afisa Progamu kutoka mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Flora Ndaba, amesema kuwa baadhi ya Taasisi hazina miundombinu rafiki ya kumsaidia mwanamke katika hali mbalimbali za kiafya anazopitia.
Aidha amesema kuwa wanawake wamekuwa na changamoto ya kuaminiwa katika baadhi ya sekta za ajira wanazopatiwa ikiwa ni pamoja na kutokupewas tahiki zao na likizo katika kipindi cha uzazi.
Taswira imezungumza na baadhi ya akina mama wanaofanya kazi katika sekta mbalimbali mkoani hapa, wamekiri kuwepo kwa changamoto ya mazingira wezeshi kazini, ambapo kwa sasa kuna ahueni ukilinganisha na hapo awali.
Dhana ya ukombozi wa mwanamke katika nyanja mbalimbali imekuwepo kwa muda mrefu Nchini, kuhakikisha sauti ya Mwanamke inasikika kuanzia ngazi ya jamii mpaka kitaifa.