Wazazi watakiwa kuwaandaa wanafunzi kurudi shule
8 January 2025, 3:34 pm
Shule za msingi na sekondari zinatarajiwa kufunguliwa Januari 13 mwaka huu, ambapo Watoto wenye umri wa kuanza shule wanatakiwa kuandikishwa.
Na Lilian Leopold .
Wito umetolewa kwa wazazi na walezi kuhakikisha wafanya maandalizi ya kutosha kwa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na shule kwa mwaka huu.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabari Shekimweri ambapo amewataka wazazi kuchukua hatua mapema za kuwaandikisha Watoto wanaojiunga na darasa la kwanza na kidato cha kwanza, pia, ameongeza kuwa ni wajibu wa kila mzazi kuhakikisha mtoto anapata elimu.
Aidha Shekimweri amebainisha lengo la Jiji la Dodoma ni kuandikisha Watoto 18, 252 wa darasa la awali lakini mpaka sasa wameandikishwa Watoto 6,893.
Kwa upande wao, baadhi ya wazazi kutoka mtaa wa Miyuji- Kibaoni wamekuwa na haya ya kusema.