Hospitali ya Benjamini Mkapa kupambana na ukatiliwa kijinsia
29 October 2024, 3:59 pm
Na Mariam Matundu.
Hospitali ya Benjamini Mkapa imeanzisha mtandao wa kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyotokea mara nyingi kwa watoto .
Hii ni kufuatia kupokea wagonjwa ambao hutibiwa hosptalini hapo na kubainika wamefanyiwa vitendo vya ukatili ama wanapitia ukatili.
Christina Mwakilasa ambaye ni muuguzi katika hospitali hiyo amesema wagonjwa wengi hawaelezi wazi vitendo vya ukatili wanavyopitia hivyo inawalazimu kujenga mahusiano ya karibu na urafiki ili kupata ukweli wa vitendo hivyo vya ukatili wanavyopitia wagonjwa hao.
Chiristina Mwakilasa mwenye tuzo ya muuguzi bora Tanzania anaeleza aina ya ukatili inayofanyika kwa kiwango kikubwa ambayo hbainika kutoka kwa wagonjwa wanao wapokea hospitalini hapo.