Dodoma FM

Wanaume tumieni dawati la jinsia kuripoti ukatili

25 September 2024, 8:26 pm

Na Lilian Leopold           

Licha ya kampeni za kupinga ukatili kufanyika hususani kwa wanawake, watoto na watu wenye ulemavu lakini wanaume wamekuwa wakisahaulika.

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Michael Nkinda

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi mkoa wa Dodoma, Michael Nkinda amesema kuwa  wanaume wengi wamekuwa wakifanyiwa ukatili wa kijinsia unaopelekea kupata ukatili wa kisaikolojia.

Sauti ya Michael Nkinda

Aidha ametoa wito kwa wanaume wanaofanyiwa ukatili kwenye jamii wasione aibu  kupaza sauti zao hasa kwenye mamlaka husika hususani katika Dawati la Jinsia ili changamoto zao ziweze kutatuliwa na kuleta usawa katika jamii.

Sauti ya Michael Nkinda

Baadhi ya wanaume jijini Dodoma wametoa maoni yao juu ya nini cha kufanya endapo wanaume wanakabiliwa na ukatikli wa kijinsia.

Sauti za wananchi

Kwa mujibu wa Ripoti ya Haki za Binadamu ya mwaka 2023, vitendo vya ukatili kwa wanaume vimeongezeka na kufikia asilimia 10, kutoka asilimia 6 ya mwaka 2022.