Jamii yakosa elimu ya kutosha juu ya utanganishaji wa taka
19 July 2024, 5:27 pm
Ili kupata matokeo mazuri ni lazima kuweka misingi ya utekelezaji ikiwa ni pamoja ushirikishwaji wa umma, utekelezaji wa sheria na makubaliano kwa wadau mbalimbali wanaojihusisha na sekta ama teknolojia ya urejelezaji taka.
Na Mariam Kasawa.
Inaelezwa kuwa Mazingira safi ni kitovu cha afya bora na maendeleo kwa wananchi Ili kufikia lengo la kuwa na mazingira safi, ni lazima kuwa na mikakati endelevu ya kudhibiti uchafuzi wa mazingira.
Ili kuweka usimamizi endelevu wa usafi Jijini ni lazima kuweka misingi ya usimamizi, tathmini na kuchukua hadhari kuhusu madhara kwa mazingira,kwa kudhibiti taka kuanzia zinapozalishwa, ukusanyaji, usafirishaji na utupaji wake.
Jiji la Dodoma linakisiwa kuzalisha tani 350 za taka ngumu kwa siku ambapo kata za nje ya mji uzalishaji tani 114 na Kata za mjini uzalisha ni tani 236 wastani wa tani 150 tu ndiyo zinaondoshwa mjini kwa siku sawa na asilimia 66%, hali hiyo imekuwa ikichangiwa na uhaba mkubwa wa vifaa hasa Skip bucket .
Katika maeneo ya masoko vifaa vya kutunzia taka vipo lakini je hali ya utenganishaji wa taka unazingatiwa.
Siku hizi katika nchi zote zilizoendelea imegundulika kuwa ni hatari na hasara kama taka zote zitatupwa mahali pamoja na kufunikwa tu bila kurejelezwa ndani ya taka kuna thamani kubwa kiuchumi Kwahiyo nchi nyingi duniani zimeanzisha taratibu za kutenganisha taka na kukukusanya kila aina ya taka peke yake.
Dickson Kimaro ni Mkuu wa Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka ngumu, yeye anaawaasa wananchi kuacha tabia ya kuchoma takataka katika mifereji na kutupa taka hovyo ni hatari kwa mazingira.
Elimu ya utenganishaji wa taka na utunzaji wa mazingira inaelezwa kuwa bado haijawafikia ipasavyo wananchi Sara Pima Mkurugenzi wa shirika la Human Diginity and Environmental care (HUDEFO) anasema elimu inapaswa kuwafikia wananchi ipasavyo ili wafahamu thamani ya kutenganisha taka.