Dodoma FM

Watoto wanaoishi mazingira magumu hatarini matumizi ya gundi, tumbaku na petrol

18 July 2024, 2:37 pm

Picha ni Dkt. Christian Bwasi Afisa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya. Picha na Mindi Joseph.

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya haitafumbia macho wauzaji wazalisha na wafadhili wa dawa za kulevya kwani wanaua nguvu kazi ya taifa.

Na Mindi Joseph.
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imeeleza kuwepo kwa wimbi kubwa la watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi kutumia gundi, petroli na mazalia ya tumbaku.
Dkt. Christian Bwasi Afisa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya anabainisha hayo huku akieleza athari wanazopata watoto hao.

Sauti ya Dkt Christian Bwasi .
Picha ni Afisa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya kanda ya Kati Anna Tengia.Picha na Mindi Joseph.

Afisa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya kanda ya Kati Anna Tengia anabainisha kuwa dawa za kulevya hazikubaliki na wamekuwa wakichukua hatua kusaidia watoto hao.

Sauti ya Bi.Anna Tengia.