Bwawa Mtwango Ndachi lainua vijana kiuchumi
18 March 2024, 12:36 pm
Mabwawa ya asili yanatumika kufugia samaki na mara nyingi bwawa la asili linaweza kupatikana ama kuwezekana kuundwa maeneo yenye udongo wa mfinyanzI na udongo huu una sifa kubwa ya kuhifadhi maji.
Na Mindi Joseph.
Uwepo wa Bwawa Mtwango katika Mtaa wa Ndachi jijini Dodoma imetajwa kuwa nguzo ya kuwainua kiuchumi vijana na wakazi wa eneo hilo.
Bwawa la Mtwango ni la asili na hutumika katika shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo cha umwagiliaji, mifugo na Ujenzi.
Miongoni mwa vijana walionufaika na bwawa hili ni Matosheki manyika ambaye anajishughulisha na kilimo cha nyanya hapa anaeleza.
Mwenyekiti wa mtaa wa Ndachi Justini Lugwalu katika mahojiano na Dodoma Tv anaeleza namna bwawa hili limekuwa mkombozi kiuchumi kwa wananchi wake.