Waganga wafawidhi watakiwa kusimamia marufuku ya simu kwa wauguzi
26 February 2024, 5:55 pm
Katika mahafali hayo jumla ya watahiniwa 2099 wameweza kutunukiwa vyeti ,kufanyiwa uorodheshwaji pamoja na pamoja na kupewa Leseni na baraza hilo la uuguzi na ukunga tayari kuanza kutumikia katika utoaji wa huduma za afya.
Na Mariam Matundu.
Waganga wafawidhi nchini wametakiwa kusimamia vyema Marufuku ya Matumizi ya Simu kwa wauguzi pamoja na wakunga wakati wa kutoa huduma ili kuboresha utoaji mzuri wa huduma za afya nchini.
Hayo yameelezwa leo na Mganga mkuu wa Serikali Prof.Tumaini Nagu wakati akizungumza katika mahafali ya 10 ya kitaaluma ya baraza la Ukunga na Uuguzi Tanzania yaliyokwenda sambamba na zoezi la ugawaji wa leseni kwa wakunga na wauguzi hao yaliofanyika leo katika ukumbi wa Mtakatifu Peter uliopo jijini hapa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza la Uguzi na Ukunga nchini Prof. Lilian Msele amewataka wauguzi na wakunga nchini kuzingatia maadili ya taalumu hiyo ili kuepuka kuingia katika mkumbo wa watoa huduma wasio na maadili.
Nao baadhi ya wahitimu katika taaluma hiyo ya uuuguzi na ukunga wameahidi kuzingatia maagizo yalitolewa na wakuu hao huku wakiahidi kwenda kufanya kazi kwa kuzingatia miiko ya kazi hiyo.