Yafahamu madhara ya utupaji taka za plastiki katika vyanzo vya maji
9 February 2024, 5:18 pm
Hata hivyo Umoja wa mataifa mara kadhaa umekuwa ukionya kuwa iwapo mataifa hayatochukua hatua za mapema kudhibiti taka zitokanazo na plastiki, huenda ulimwengu ukashuhudia idadi kubwa ya plastiki katika maziwa na bahari ukilinganisha na Samaki ifikapo mwaka 2050.
Na Mariam Kasawa.
Utupaji wa taka za plastiki hususani chupa kwenye maji yanayo tiririka inatajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa unaribufu wa mazingira na uhai wa viumbe hai.
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Zaidi ya tani milioni 400 za plastiki huzalishwa kila mwaka kote duniani, nusu ya taka hizo hutumika tu mara moja, Kati ya hizo, chini ya asilimia 10 ya plastiki huchakatwa, na kila mwaka takriban tani kati ya milioni 19 na milioni 23 huelekea kwenye Maziwa, Mito na Bahari.
Uchafuzi huo wa mazingira ni mwiba mkali kwa viumbe hai waishio chini ya maji kutokana na taka ngumu kama plastiki kutiririshwa baharini, mitoni na maeneo ya ziwani hivyo kuendelea kuhatarisha Maisha ya Samaki ambao kwa sasa wapo hatarini kutoweka.
Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) katika ripoti yake ya mwaka 2022 ilieleza kuwa idadi ya uchafu wa plastiki inayoingia kwenye mifumo ya ekolojia ya majini imeongezeka kwa miaka ya hivi karibuni na inakadiriwa kuongezeka maradufu kufikia mwaka wa 2030.
Umewahi kujiuliza taka hizi za plastiki zinazotupwa katika maji yanayo tiririka huwa zinakwenda wapi msikilize Sara pima mkurugenzi na mdau wa mazingira kutoka shirika lisilo la kiserikali la utunzaji mazingira HUDEFO.
Isaya Silungwe ni Mkurugenzi wa Youth Forum asasi inayo jihusisha na utunzaji wa mazingira Jijini Dodoma yeye anasema uchakataji wa taka za plastiki unasaidia sana kulinda mazingira.
Ripoti ya UNEP ya mwaka 2021 inaonesha kwamba plastiki huchangia asilimia 85 ya takataka za baharini na inaonya kuwa kufikia mwaka wa 2040, kiwango cha uchafu wa plastiki katika maeneo ya baharini kitaongezeka karibu mara tatu.