Wananchi wajitokeza kuchimba Msingi ujenzi wa Madarasa Bahi
8 May 2023, 1:51 pm
Wakazi wa kijiji cha Bahi sokoni wameeleza kupokea mradi huo kwa furaha na kuiomba serikali kuendelea kupeleka miradi ya maendeleo katika kijiji hicho.
Na Bernad Magawa.
Wananchi wa kijiji cha Bahi Sokoni wilayani Bahi wamejitokeza kwa wingi kuchimba msingi wa Madarasa na Jengo la utawala katika shule ya msingi Bahi Misheni kama sehemu ya wao kuunga mkono juhudi za serikali kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa katika shule hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya serikali, Mkuu wa idara elimu ya Awali na msingi wilaya ya Bahi Boniphace Wilson amesema ujenzi wa madarasa hayo ni sehemu ya mkakati wa serikali kuhakikisha inapunguza msongamano wa watoto madarasani.
Naye Diwani wa kata ya Bahi Agostino Ndonu amesema uongozi na wananchi wa kata ya Bahi wamejipanga kikamilifu kuhakikisha miradi iliyopo kwenye kata hiyo inakamilika kwa wakati kadiri ilivyopangwa huku akieleza majukumu ya wanachi kwenye miradi hiyo.
Katika hatua nyingine wananchi wa kijiji cha Bahi sokoni wameeleza kupokea mradi huo kwa furaha na kuiomba serikali kuendelea kupeleka miradi ya maendeleo katika kijiji hicho ambacho ndipo yalipo makao makuu ya wilaya ili kuendelea kusogeza zaidi huduma kwa wananchi.