Wanachama wa WAUVI waanza uzalishaji wa bidhaa
2 May 2023, 12:21 pm
Mafunzo hayo yamekuwa yakiratibiwa na shirika la kuhudumia viwanda vidogo sido mkoa wa Dodoma.
Na Alfred Bulahya.
Imeelezwa kuwa asilimia 80 ya wanachama wa Taasisi ya wanawake na Uchumi wa Viwanda wilaya ya Dodoma Mjini WAUVI wameanza kufanya uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kupitia viwanda vidogo baada ya kupatiwa mafunzo.
Akizungumza katika mkutano maalumu na wanachama hao Mkufunzi kutoka shirika la kuhudumia viwanda vidogo Mkoa wa Dodoma SIDO Maurasa Shoo amesema asilimia 80 wameanza uzalishaji wa sabuni na asilimia 65 wameanza kutengeneza batiki.
Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Dodoma, Getrude Izengo, akawataka akin mama katika taasisi kuacha kusahau majukumu ya kulea familia ili kupunguza kumomoyoka kwa maadili.