Walimu watakiwa kuzuia maudhui yasiyofaa
13 April 2023, 5:08 pm
Jiji la Dodoma limetakiwa kutenga fedha na kuongeza vifaa vya Tehama kwa shule kwa lengo la kuendelea kuboresha ujifunzaji wa wanafunzi shuleni.
Na Mindi Joseph.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabiri Shekimweri amewataka walimu wanaosimamia Tehama kufuatilia kwa karibu maudhui yanayowekwa kwenye vishikwambi na kuzuia maudhui yasiyofaa kwa wanafunzi.
Ameyabainisha hayo leo jijini Dodoma katika uzinduzi wa Mradi wa kukabidhi vifaa vya tehema uliofanyika katika shule ya Miyuji sekondari vifaa hivyo vitumike kwa malengo yaliyokisudiwa na viwe na usimamizi unaostahili.
Kwa upande wake Mkurugenzi African Child Projects mradi wa kuunganisha shule na internet Catherine Kimambo amesema milion 48 zimetumika katika shule tisa za Dodoma.
Naye Mkuu wa kanda ya kati Voodacom Joseph Sayi amebainisha kuwa wanafunzi laki 6 wamenufaika na mpango wa uunganishaji wa mtandao nchini.