Serikali yatenga billioni 15 kwaajili ya kukamilishaji zahanati 300
5 April 2023, 5:57 pm
Mbunge wa Jimbo la Rorya, Mhe. Jafari Wambura alitaka kujua Je, nini mpango wa Serikali wa kumaliza ujenzi wa Zahanati kwa vijiji vilivyokamilisha ujenzi wa maboma.
Na Pius Jayunga.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange amesema katika mwaka wa fedha 2022/23 Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 15 kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma ya zahanati 300, hadi kufikia Februari 2023 kiasi cha shilingi bilioni 14.6 zimekwishatolewa.
Amesema hayo tarehe 05 Aprili 2023 Bugeni Dodoma wakati akijibu Swali la Mbunge wa Jimbo la Rorya, Mhe. Jafari Wambura aliyetaka kujua Je, nini mpango wa Serikali kumaliza ujenzi wa Zahanati kwa vijiji vilivyokamilisha ujenzi wa maboma.
Katika kikao hicho mbunge wa jimbo la chemba Mohamed moni amehoji ni lini serikali itakamilisha ujenzi wa boma zahanati ya isusumya licha ya kupelekwa ombi maalumu.