Madereva bajaji Jamatini B wajivunia mshikamano wao
31 March 2023, 7:07 pm
Na Thadei Tesha
Madereva wa bajaji katika kituo cha Jamatini B jijini Dodoma wamesema kufanya kazi kwa umoja kama kikundi kumewasaidia kupata fursa zaidi kupitia biashara yao.
Hapa ni katika kituo cha bajaji cha Jamatini b nafika na kuzungumza na baadhi ya vijana ambao wameamua kujiajiri kupitia biashara ya kuendesha bajaji.
Naanza kwa kuwauliza biashara hii imewasaidia vipi kujikwamua kiuchumi lakini pia wananufaika vipi baada ya kuunda umoja wao kama madereva bajaji?
Usafiri huu wa bajaji unatajwa kurahisisha shughuli mbalimbali hususani kutoka eneo moja kwenda eneo jingine na hapa baadhi ya wananchi wanaeleza kwanini hupendelea kutumia usafiri wa bajaji?
Katika jiji la Dodoma ipo mitaa ambayo usafiri mkubwa kwao ni pamoja na bajaji ambapo miongoni mwa mitaa hiyo ni pamoja na makulu sambamba na mtaa wa kikuyu.