Tumieni teknolojia vizuri kukuza uchumi
26 February 2021, 9:15 am
Na, Benard Philbert,
Dodoma.
Jamii imeshauriwa kutumia teknolojia ipasavyo ili kutambua fursa mbalimbali zitakazo changia katika ukuaji wa uchumi.
Hayo yameelezwa na mhandisi Eliponda Hamir kutoka taasisi ya Teknolojia Tanzania Community network, wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu matumizi ya teknolojia katika kukuza uchumi kwa wananchi.
Mhandisi Eliponda amesema hivi sasa kwa mtu yeyote ambaye anahitaji kukua kiuchumi ni vyema akaendana na mabadiliko ya teknolojia, kwani ina nafasi kubwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Ameongeza kuwa teknolojia inaongeza fursa kwa kiasi kikubwa kutokana na kuunganisha watu katika maeneo tofauti hali inayosaidia kuongeza mnyororo wa thamani kwa wana nchi.
Baadhi ya wananchi jijini Dodoma wakizungumza na taswira ya habari, wamesema ni kweli ili kukuwa kiuchumi kwa mwananchi mmoja mmoja na nchi kiujumla ni muhimu kuendana na teknolojia na sio vinginevyo.