Ukosefu wa elimu juu ya mikopo waleta changamoto ya urejeshaji wa mikopo
5 April 2022, 2:22 pm
Na; victor Chigwada.
Pamoja na kasi ya uundwaji wa vikundi vya vijana na wajasiriamali mabalimbali nchini ambavyo hupatiwa mikopo ya kuendesha shughuli zao lakini kumekuwa na changamoto ya upataji wa elimu juu ya mikopo hiyo pamoja na matumizi yenye tija.
Afisa maendeleo ya jamii katika kijiji cha Mlebe Bi.Ng’washi Muhuli amesema kuwa kumekuwa na changamoto ya urejeshaji mikopo hiyo licha ya baadhi ya vikundi vya wanawake kufanya vizuri.
Aidha Bi.Muhuli ameongeza kuwa kumekuwa na mashirika mbaimballi yanayo jitokeza katika kutoa elimu juu ya vikundi hususani katika kujishughulisha na shughuli mbalimbali lakini nayo yamekuwa yakishindwa kwenda na wakati.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mlebe Bw.Joseph Mpilimi amewaasa vijana na vikundi mbalimbali kuhakikisha wanakuwa na shughuli maalumu za kufanya ili kuepuka adha ya kudaiwa kutokana na mikopo wanayo chukua
Vikundi vya ujasiriamali vimekuwa na tija kwa jamii na kupelekea kujikwamua kiuchumi na kkubadilisha maisha ya mtu mmoja mmoja