Ukosefu wa lishe bora kwa watoto watajwa kusababisha ongezeko la udumavu na utapiamlo
21 October 2021, 12:07 pm
Na; Fred Cheti.
Ukosefu wa lishe bora kwa watoto nchini unatajwa kuwa chanzo cha kuongezeka kwa udumavu wa akili pamoja na ugonjwa wa utapiamlo jambo ambalo hupunguza uwezo wa kufanya vizuri shuleni pamoja na ufanisi katika maisha ya utu uzima.
Tafiti hiyo ni kulingana na taasisi ya lishe na chakula nchini ambayo inaeleza kuwa zaidi ya watoto milioni tatu( 3) wa Tanzania wenye umri chini ya miaka 2 wamedumaa kutokana na kukosa chakula cha kutosha.
Baadhi ya wazazi jijini hapa wamezungumza na taswira ya habari juu ya sababu zinazosabisha watoto wengi kutopatiwa mlo kamili jambo ambalo husababisha kukumbwa na matatizo hayo.
CLIP 1….WAZAZI UTAPIAMLO
Kwa upande wake Afisha Lishe wa halmashauri wa jiji la Dodoma Semieva Juma anasema halmashauri ya jiji kupitia idara ya afya kitengo cha lishe imekuwa ikishirikiana na wadau mabalimbali wa afya katika kutoa elimu kwa jamii kuhusina na lishe bora kwa mtoto.
CLIP 2..AFISA LISHE JIJI
Kiwango cha udumavu Tanzania ni zaidi au karibu sawa na asilimia 40 kwa watu wazima wote isipokuwa tu kwa wenye vipato vya juu wachache wanaokadiriwa kuwa takribani asilimia 20. Ushahidi huu unaashiria kwamba chanzo hasa cha udumavu ni zaidi ya upungufu wa chakula na umaskini wa familia.