Ongezeko la watu wilayani Bahi lapelekea uhita wa maji zaidi
17 September 2021, 1:44 pm
Na; Benard Filbert.
Licha ya mji wa Bahi Mkoani Dodoma kupokea fedha kiasi cha shilingi million 120 kwa ajili ya kuchimba kisima kipya ili kuongeza upatikanaji wa maji bado juhudi zinahitajika kutokana na wingi wa watu katika eneo hilo.
Hayo yameelezwa na Diwani wa kata ya Bahi Bw. Agustino Leonard wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu hali ya upatikanaji wa maji katika kata ya Bahi.
Bwana Leonard ameiambia taswira ya habari kuwa hivi karibuni Serikali imetoa fedha million 120 lengo ikiwa ni kuchimba kisima kipya cha maji kutokana na ongezeko la watu katika mji huo.
Akizungumzia kuhusu kuboresha huduma ya maji kutokana na vyanzo vilivyopo amesema wanategemea bajeti zitakazopatikana kutoka DUWASA kwani ndio wenye mamlaka ya kufanya hivyo.
Kadhalika amesema kuwa toka mji huo uanze kuhudumiwa na DUWASA kumekuwa na afadhali kwani kero ya upatikanaji wa maji imepungua.