Uzalishaji wa maji taka umekuwa sababu ya kuharibu mazingira
30 August 2021, 1:50 pm
Na;Yussuph hans,
Uzalishaji uliokithiri wa majitaka umekuwa sababu kubwa ya kuharibika kwa mazingira pamoja na chanzo cha maradhi mbalimbali ya mlipuko katika jamii.
Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya Wakazi Mkoani Dodoma wamesema kuwa jamii imekuwa na ufahamu kuhusu madhara ya Maji taka kwa kiasi huku bado elimu ya madhara hayo inahitajika zaidi.
Wameongeza kuwa kumekuwa na desturi ya utiririshaji maji taka katika kipindi cha mvua suala husababisha uchafuzi wa Mazingira katika vyanzo vya Maji.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Maji na usafi wa Mazingira Mkoani Dodoma DUWASA amesema wamekuwa desturi kushughulikia changamoto hizo huku akibainisha changamoto iliyopo ni matumizi ambayo sio rafiki ya utupaji taka ngumu katika chemba za maji.
Usambaaji wa maji taka katika mitaa kutokana na kuzibuka kwa chemba za una athari athari mbalimbali pindi yanapongia katika jamii, Uzalishaji uliokithiri wa majitaka umekuwa sababu kubwa ya kuharibiwa kwa mazingira na kusababisha maradhi mbalimbali ya mlipuko.