Imeelezwa kuwa migogoro ya ardhi ni sababu inayo pelekea baadhi ya watu kushindwa kufanya kazi
16 July 2021, 11:36 am
Na; Sani Nicolous.
Pamoja na kwamba serikali bado inaendelea na kampeni ya kutatua migogoro ya ardhi lakini kuna baadhi ya maeneo wakulima na wafugali wapo katika migogoro mikali ya ardhi.
Akizungumza na Dodoma fm Diwani wa kata ya Mpendo wilaya ya Chemba Bw.Benard Kapaya amesema kuwa kuna eneo linagombaniwa na wananchi katika kijiji cha Kubi ambapo serikali ya kijiji hicho imejaribu kufanya mikutano kutatua mgogoro huo imeshindwa hivyo ofisi yake inasubiri taarifa maalum ili iweze kuingilia na kutatua mgogoro huo.
Aidha amesema kuwa migogoro ya ardhi hupelekea watu kuto kufanya kazi badala yake wanatumia muda mwingi kuzunguka huku na huko ili kutafuta jinsi ya kushindana katika kesi ya kugombania ardhi.
Amesema ni vyema watu wakatambu umuhimu wakufanya kazi kwa bidii na kuacha kupoteza muda kwa kuendekeza migogoro kwani serikali tayari imetenga muda kwaajili ya mkoa mzima kusikiliza na kutatua changamoto za migogoro ya ardhi kupitia kampeni ya (zero migogoro ya ardhi).
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Mh. Jabiri Shekimweri amesema kuwa baada ya kutambua kwamba kuna watu hawakufikiwa na kampeni hiyo wamefanya majadiliano na Mkuu wa Mkoa pamoja na wizara husika kuongeza siku ambapo itakuwa mwezi mzima na utaratibu utatolewa kwa mkoa mzima
Nikipindi kirefu baadhi ya wanachi mkoani Dodoma wamekuwa na kiu ya kumaliza changamoto mbalimbali za migogoro ya ardhi na serikali inaendelea kushughulikia changamoto hiyo hivyo wakazi wa kata ya Mpendo wajiandae kutoa ushirikiano kwa serikali endapo wakifika katika maeneo yao.