Ukosefu wa Elimu ni kikwazo kwa wazalishaji wadogo wa bidhaa Nchini
9 July 2021, 11:44 am
Na; Shani Nicolous.
Ukosefu wa elimu na jinsi ya kupata soko kwa wazalishaji wadogo wa bidhaa Nchini imetajwa kuwa changamoto hivyo kushindwa kuongeza mnyororo wa thamani.
Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mtendaji wa jukwaa la wadau wa sekta ya kilimo Bw. Oudax Ukonge wakati akizungumza na kituo hiki na kusema wazalishaji wadogo wanashindwa kufikia malengo yao katika sekta ya kilimo kutokana na ukoseu wa elimu juu ya utafutaji masoko ya mazao yao.
Amesema kuwa ni vema wakulima kuto subiri Serikali kufanya kitu kwa ajili yao bali waanze kufanya jambo litakalokuwa na hamasa kwa viongozi mbalimbali katika sekta hiyo kufanya jambo kwa ajili ya kuwaendeleza
Ameeleza kuwa wapo baadhi ya vijana ambao tayari wamekuwa na mwamko wa kufanya kujituma katika shughuli za kilimo na wameanza kupata matoke mazuri kupitia sekta hiyo.
Baadhi ya wananchi Jijini Dodoma wamesema kuwa utoaji wa elimu juu ya kilimo chenye tija inamchango mkubwa kwa wakulima wadogo wadogo hasa maeneo ya Vijijini kwani itasaidia kuachana na kilimo cha mazoea na hata kuongeza thamani ya mazao katika sekta ya kilimo Nchini.
Sekta ya kilimo ni kati ya sekta muhimu inayoweza kuchangia pato la Taifa kwa asilimia kubwa ikiwemo kuongeza ajira na hata kuwaongezea kipato Watanzania endapo itatendewa haki kwa baadhi ya changamoto zinazoikabili sekta hiyo.