Uhaba wa maji wapelekea wakazi wa Lugala kushea vyanzo vya maji na wanyama
1 July 2021, 6:20 am
Na; Benard Filbert.
Afya za Wakazi wa Mtaa wa Lugala jijini Dodoma zipo hatarini kutokana na kutumia vyanzo vya maji pamoja na wanyama.
Uhaba wa upatikanaji wa huduma ya maji katika mtaa huo ndio imepelekea wakazi hao kufanya hivyo.
Wakizungumza na taswira ya habari Wamesema kitendo cha kutumia visima hivyo pamoja na wanyama hakuna usalama wa kiafya jambo ambalo ni hatari kwao.
Zephania Mgutwa ni mwenyekiti wa mtaa wa Lugala amekiri kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa maji kwa muda mrefu.
Ameongeeza kuwa athari ambazo wamekuwa wakikutana nazo wakazi wa mtaa huo ni kubwa kutokana na kupoteza muda mwingi kutafta maji.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Mbalawala Charles Zephania amesema chanagamoto iliyopo katika kata hiyo ni miundombinu ya maji kuharibika kutokana na marekebisho ya barabara lakini hivi karibuni wanatarajia kutatua kero hiyo.
Kutokutumia maji safi na salama inaweza kusababisha magonjwa mbalimbali ikiwepo homa za matumbo.