Wizara ya Afya yazindua mpango mkakati wa miaka mitano utakao gharimu shilingi trilioni 9.4
24 June 2021, 1:44 pm
Na;Mindi Joseph.
Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii jinsia,wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo,imezindua mpango mkakati wa miaka mitano utakaogharimu Tsh.Trilioni 9.4 kila mwaka.
Akizungumza katika uzinduzi mkakati huo leo Juni, 24,2021 Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii jinsia ,wazee na Watoto Dokta Dorothy Gwajima katika mpango huo Tsh.Trilioni 9.4 zitatumika katika mpango huo kwa kila mwaka ambapo ni sawa na Tsh.Trilioni 47 kwa kipindi chote cha miaka mitano.
Katika utekelezaji wa mpango huo Dkt.Gwajima amehimiza wadau wa Maendeleo kuendelea kuchangia pamoja na kutoa rai kwa menejment ya utumishi wa umma kusimamia kikamilifu mpango huo.
Dokta Gwajima ameainisha maeneo ya matokeo ya mkakati kuwa ni pamoja na kuboresha utoaji wa huduma za afya kulingana na mahitaji,kuimarisha utayari wa kujiandaa na kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ,kuimarisha uhusiano wenye matokeo chanya mifumo ya Afya.
Katika hatua nyingine,Dokta Gwajima amesema bado kuna changamoto ya watanzania kutokuwa na mwamko wa bima ya Afya ambapo ni asilimia 14 tu ya watanzania Wana bima ya Afya.
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani(WHO) nchini Tanzania Dkt Tigest Ketsela Mengestu amesema wao Kama wadau wa Maendeleo wataendelea kusaidia serikali ya Tanzania huku mwakilishi wa USAID Tanzania Andy Karas akisema mpango huo utasaidia kupunguza vifo vya akina mama na Watoto.