Jumla ya wakazi 3000 wanatarajia kupata ajira kupitia ujenzi wa kiwanda cha mbolea
3 June 2021, 2:13 pm
Na;Mindi Joseph.
Jumla ya wananchi elfu 3000 wanatarajia kupata ajira kupitia ujenzi wa kiwanda cha mbolea Nala jijini Dodoma huku wananchi wa eneo hilo wakitarajia kunufaika zaidi na uboreshwaji wa miundombinu ya umeme na maji.
Taswira ya habari imezungumza na, Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kanda ya Kati, Dodoma. Bw. Abubakari Ndwata ambaye amesema wananchi wa kijiji cha Nala watanufaika Zaidi kwani tayari eneo hilo limeunganishwa umeme na kuchimbwa visima vya maji ambapo kimoja kimekamilika huku kimoja kikiendelea kuchimbwa.
Ameongeza kuwa kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda cha mbolea itasaidia kuonkoa fedha zinazotumika kuagiza mbolea nje ya nchi ambapo Tanzania inaagiza karibu tani laki saba na kiwanda hicho kitazalisha tani laki tano kwa mwaka.
Kwa upande wake Mhandisi wa Mradi Tumaini Chonya kutoka Tanesco Dodoma amebainisha kuwa uwekaji wa umeme katika Eneo la Nala umefikia asilimia 95 ndani ya siku saba.
Naye Mwekezaji wa mradi wa Intracom kutoka Burudi mhandisi Musafiri Dieudonne amekipongez kituo cha uwekezaji Tanzania TIC na Tanesco kwa jitihada kubwa ya kuweka miundombinu ya umeme na maji na kuanzia wiki ijayo ujenzi wa kiwanda hicho unatarajiwa kuanza.
Ujenzi wa kiwanda cha mbolea Nala unatarajiwa kukamilika ndani ya Miezi 9 kupitia kampuni ya intracom na kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani laki tano na ujenzi huo utagharimu takribani dola za Marekani million 180.