Serikali yaweka mkakati ujenzi wa viwanda ili kupunguza Tatizo la ajira Nchini
27 May 2021, 2:53 pm
Na; Yussuph Hans.
Kufuatia changamoto ya upatikanaji wa Ajira kwa Wahitimu Nchini, Serikali inaweka utaratibu mzuri ikiwemo mkakati wa ujenzi wa viwanda ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto hiy
Hayo yamebainishwa leo Bungeni Jijini Dodoma na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Kassim Majaliwa wakati akijibu swali la Mbunge wa Singida Mh Nusrat Shaaban Hanje aliyehoji nini mkakati wa Serikali kusaidia vijana kupata ajira hasa waliomaliza Darasa la Saba na kujiendeleza katika vyuo vya ufundi Nchini.
Mh Majaliwa amesema kuwa serikali inaendeleza mkakati wa awamu ya tano unaoridhia Mhitimu mwenye ujuzi kutapata ajira bila ya kujali kiwango chake cha elimu.
Ameongeza kuwa kwa sasa Serikali inaendelea kuimarisha mfumo wa elimu kwa vyuo vya ufundi stadi, ili wahitimu kuweza kujiajiri na kutoa Ajira kwa wengine.
Kwa upande mwengine Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akijibu swali la Mbunge wa Makete Mh Festo Sanga aliyehoji serikali ina mkakati gani kuzuia vitendo vya kijambazi zinavyozidi kushamiri baadhi ya maeneo Nchini, na kuhatarisha Usalama wa Wananchi pamoja na mali zao.
Mh Majaliwa amesema Vyombo vya Ulinzi na Usalama vimeagizwa kuchukua hatua kali dhidi ya wanaosababisha madhara ya kiusalama. Pia ameeleza, mara kadhaa Watanzania wameombwa kushiriki kwenye ulinzi wa Nchi.
Sanjari na hayo Wizara ya Mifugo na Uvuvi imewasilishwa Bajeti yake leo Bungeni Jijini Dodoma kwa mwaka wa fedha 2021/22.