Wakazi wa kata ya Keikei walalamikia kukosa huduma ya maji.
20 May 2021, 1:44 pm
Na ;Benard Filbert.
Uchakavu wa miundombinu ya maji katika Kata ya Keikei Wilayani Kondoa imetajwa kuwa sababu inayochangia kukosekana kwa huduma ya maji.
Hayo yameelezwa na baadhi ya wakazi wa Kata hiyo wakati wakizungumza na taswira ya habari kuhusu sababu za kukosekana kwa huduma ya maji katika Kata hiyo.
Wamesema changamoto hiyo ni ya muda mrefu kwani maji ambayo yanatoka hayakidhi mahitaji huku wengine wakichota kwenye visima vichafu.
Wameiomba Serikali kuipa kipaumbele Kata ya yao kwa kuwawekea miundombinu mingine itakayoweza kuwafikishiahuduma ya maji na kuwaondolea adha hiyo.
Mchana Issa Tesi ni Diwani wa Kata ya Keikei amesema ni kweli kuna changamoto ya ubovu wa miundombinu ya maji na suala hilo tayari amelifikisha kwenye vikao vya Halmashauri hivyo anatarajia tarehe 27 mwezi huu watapatiwa majibu juu ya marekebisho ya miundombinu hiyo.