Waziri mkuu azindua vitabu vya miongozo ya utayarishaji wa miradi ya maji
12 May 2021, 10:12 am
Na; Mindi Joseph
waziri mkuu kasimu majaliwa amezindua vitabu vya miongozo ya utayarishaji wa miradi ya maji ili kupunguza changamoto ya maji nchini.
Akizungumza baada ya kuzindua mwongozo huo Kwenye kikao cha watendaji wa sekta ya maji nchini LEO jijini Dodoma waziri mkuu amewaagiza mawaziri wa wizara ya maji na TAMISEMI kuhakikisha wanasimamia upatikanaji wa maji kwakuwa wizara hizo mbili zinafanyakazi kwa pamoja katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za maji safi na salama.
Aidha amewaagiza mawaziri hao kusimamia vyema na kwa uadilifu rasilimali fedha zinazokusanywa kwenye Ankara za maji ilikudhibiti mianya ya rushwa kwa baadhi ya watendaji wasio waaminifu.
Hata hivyo waziri mkuu ametoa wito kwa wafanyakazi wa sekta ya maji kufanya Kazi kwa uzalendo na kuongea bidii ilikufikia malengo waliojiwekea huku akiwaagiza watendaji wa sekta ya maji nchi Kutoa elimu kwa wananchi namna ya kutunza vyanzo vya maji ikiwemo kupanda miti katika vyazo vya maji ilikupunguza upotevu wa maji na kutunza mazingira na watakaoonekana kuharibu vyanzo hivyo kwa shughuli mbalimbali ikiwema shughuli za kilimo wachukuliwe hatua Kali.
Naye Waziri wa maji Jumaa Aweso amesema lengo la kuandaa miongozo hiyo ni kuhakikisha wanatatua changamoto za maji nchini kwani kumekuwepo na changamoto ya upatikanaji wa maji kutokana na utengenezaji mbaya wa miradi ya maji hivyo miongozo hiyo itawasaidia wataalamu kutengeneza miradi mizuri.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya kilimo,Mifugo na Maji Christina Ishengoma ameiomba wizara ya maji kuweka mikakati thabiti ya kuvuna maji ya mvua yanayopotea chini ambapo amesema wananchi wakielimishwa jinsi ya kuvuna maji ya mvua msimu unapofika hapatakuwa na changamoto ya maji nchini huku waziri wa TAMISEMI Mh ummy mwalimu,amebainisha kuwa atashirikiana kwa dhati na wizara ya maji katika kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana katika kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya maji nchini inakamilika ili wananchi wanufaike na maji hayo.
Kaulimbiu ya kikao cha watendaji wa sekta ya maji ni tulipotoka,tulipo na tunapoelekea.