Jamii imetakiwa kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum.
6 May 2021, 1:56 pm
Na; Benard Filbert.
Jamii inaaswa kutoa msaada kwa watu wenye mahitaji maalumu ikiwepo watoto wanaoishi katika mazingira magumu hali itakayosaidia kukidhi mahitaji yao ya msingi.
Wito huo umetolewa na mratibu wa shirika la Charity Vision Tanzania Mariam Mbijima mara baada ya kukabidhi sukari pamoja na unga kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Hombolo bwawani .
Bi Mariam amesema lengo la kutoa msaada huo katika shule hiyo ni kutokana na kuguswa kufuatia wanafunzi hao kukosa chakula.
Aidha amesema kutoa ni moyo kwani kuna makundi katika jamii hayana uwezo wa kutafuta chakula hivyo kwa wale wenye uwezo wanatakiwa wajitokeze kutoa msaada.
Naye mwalimu mkuu shule ya msingi Hombolo bwawani bwana Robert Luambano ameishukuru taasisi ya charity vision kwa msaada huo kwani msaada huo utawasaidi kwa kiwango kikubwa.
Taasisi ya Charity Vision Tanzania imekuwa ikitoa msaada wa vifaa vya macho katika hospitali mbalimbali lengo kukabiliana na matatizo ya macho katika jamii.