Dodoma FM

Afisa Misitu mbaroni kwa tuhuma za rushwa

17 January 2025, 5:31 pm

Picha ni Mahakama ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara.Picha na Kitana Hamis.

Mahakama isikilize kesi hizo kwa haraka ili Wananchi Wazee kupata Haki zao kwa haraka na kwa usahihi Zaidi kwasababu inavyokuwa inachukuwa zaidi mda Mrefu unakuta mwananchi anapoteza Mda Mwingi pia haki yake inachelewa Kupatikana.

Na Kitana Hamis.
Afisa misitu wa Suluedo Wilayani Kiteto Mkoani Manyara amepandishwa kizimbani baada ya kukutwa na tuhuma za kupokea rushwa ya kiasi cha shilingi laki 6.

Akisoma shitaka hilo namba tatu (3) la Mwaka 2025 Mbele ya Mahakama ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara Mwendesha mashitaka wa Takukuru Yahaya Mzee Kileja amemtaja Mtuhumiwa kwa jina kuwa ni slomo Manyindo mtero Miaka Thelathini na mbili (32) .

Amesema Mshitakiwa. Huyo ametenda Kosa hilo Kinyume na kifugo cha Kumi na Tano (15) kifugo kidogo Cha kwaza A chasheria ya kupambana na rushwa Sura 229 Kama ilivyo fanyiwa Marejeo 2022.

Amesema mshitakiwa kwa Makusudi akijua kuwa nikosa Kisheria December 16 /2024 Huko katika Maeneo ya Kata ya Sunya aliomba Rushwa Kiasi Cha Sh: laki sita ili atoe Ruhusa kwa Mwenyekiti wa Kitongoji Cha Asamatwa alime ndani ya Msitu wa Suledo Kinyume cha Sheria.

Picha ni Msitu wa Suledo unaopatikana wilayani Kiteto mkoani Manyara.Picha na Kitana Hamis.

Kufuatia madai hayo kikosi cha Kupambana na Rushwa Takukuru hapa Wilaya Kiteto Kikaweka Mtego kwa Mtuhumiwa huyo Kisha kumkamata December 17 / 2024 akiwa na kiasi cha Elfu Tisini (90).

Hata hivyo Mtuhumiwa huyo Mbele ya Hakimu lusiyoki alikana shitaka lake hilo Kisha Kurejeshwa Rumande bada ya kukosa Thaman a ya kutokidhi mashariti ya Mahakama hio.

Hiyo shauri hili limepagwa tena kusikilizwa January/ 28/2025 nje ya Mahakama dodoma fm tumezungumza na Baadhi ya Wananchi kuhusu Kesi hii.