Dodoma FM

Vijana 420 kushiriki mrapi wa BBT awamu yapili

14 January 2025, 11:47 am

Hadi sasa wameshapokea vijana 209 na bado wanaendelea kuwasili ili kufikia idadi hiyo ya vijana katika shamba hilo ambalo ni awamu ya pili ya vijana kuwasili.Picha na Michuzi blog.

Hata hivyo amesema maandalizi kwa ajili ya kiwapokea vijana hao yamekamilika ambapo alisema katika shamba hilo kila kitu ambacho kinahitajika kwa ajili ya kilimo kipo kwa ajili ya kuanza uzalishaji.

Na Selemani Kodima.
Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imeanza kuwapokea vijana wa awamu ya pili wa Mradi wa Jenga Kesho iliyo Bora (BBT), ambapo 420 kutoka mikoa mbalimbali nchini watashiriki.

Akizungumza , Januari 12, Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango na Bajeti wa Wizara ya Kilimo, Mohamed Chikawe amesema awamu hii inalenga kuzalisha zaidi ya tani 8,400 za mbegu bora ya mahindi aina ya C105 kwenye ekari 4,200 zilizotengwa kwa mradi huo.

Sauti ya Mohamed Chikawe.

Vijana hao wanatarajiwa kufanyia kazi katika eneo maalumu la Ndogoye, lililopo wilayani Chamwino, mkoani Dodoma. Mradi huu ni sehemu ya juhudi za Serikali kuimarisha sekta ya kilimo, kuongeza uzalishaji wa mbegu bora, na kuwajengea vijana uwezo wa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya kilimo.