Wananchi wanajikingaje na ajali za barabarani?
6 January 2025, 1:30 pm
Ajali za barabarani kuanzia Januari hadi Desemba mwaka 2024 zilikuwa 1,735, huku ajali 1,198 zilisababisha vifo vya watu 1,715.
Na Lilian Leopord.
Kuzingatia alama za Barababani na uendeshaji salama ni miongoni mwa tahadhari zinazochukuliwa na baadhi ya madereva wa vyombo vya moto na kuwakinga wengine na ajali za barabarani Jijini Dodoma.
Wakifanya mahojiano na Dodoma Tv, wananchi wa mtaa wa Miyuji- Kibaoni Wananchi jijini Dodoma wameelezea hayo ikiwa ni hatua wanazochukuwa kujikinga na ajali za barabarani.
Akizungumza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akitoa salamu za krismass na mwaka mpya akiwa Ikulu, Disemba 31 amesema ajali za barabarani kuanzia Januari hadi Disemba mwaka 2024 zilikuwa 1735, huku ajali 1198 zilisababisha vifo vya watu 1715. Na ameongeza kuwa asilimia 97 ya ajali zimetokana na uzembe wa madereva.