Mhandisi mradi wa Tactic atakiwa kukamilisha kazi kwa wakati
6 December 2024, 11:26 am
Maandalizi ya utekelezaji wa mradi huu yamegawanywa katika makundi matatu kwa kuzingatia awamu za mgao wa fedha kutoka kwa mfadhili (Benki ya Dunia).
Na Annuary Shaban.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Alhaj Jabir Shekimweli amemtaka mhandishi wa mradi wa tactic kuhakiksha anasimamia ipasavyo ili mradi huo ukamilike kwa wakati.
Ameyasema hayo wakati wa akikagua mradi huo wa tactic ambapo amesema ili kukamilika kwa mradi mhandisi anapaswa kuhakikisha kuwa mikataba ya malipo inakamilika kwa wakati.
Kwa upande wake Mhandisi wa jiji la Dodoma Nikodemous Kileo amesema mradi huo utahusisha masoko vivuko salama Pamoja na stendi .
Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma ni miongoni mwa Miji 45 ambayo imepewa kipaumbele cha kupata ufadhili wa mradi huu wa uboreshaji miundombinu ya Miji, Manispaa na Majiji.