Dodoma FM

Paranga Chemba walilia zahanati

14 November 2024, 8:06 pm

Na Yussuph Hassan,

Wakazi wa kijiji cha Paranga Wilayani Chemba Mkoani Dodoma wapo tayari kuchangia nguvu zao ili kufanikisha ujenzi wa zahanati  ili kuondokana na changamoto ya wanawake kujifungulia njiani.

Hatua hii inajiri baada ya kufikiwa na mradi wa ninawajibika unaotekelezwa na taasisi ya Wajibu kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la AFNET ,lengo likiwa ni ushiriki wa  wananchi katika miradi ya maendeleo

Baadhi ya wanawake akiwemo Aisha Salum,Maria Tula na Halima Abdalah wamesema  kutokana na ukosefu wa zahanati kijijini inalazimu kutumia dawa za miti shamba ili kupata ahueni ya matibabu.

Pichani moja wa mwananchi akieleza athari zinazowakabili kutokana na kukosekana kwa zahanati Peranga Chemba
Sauti za wananchi

Fatma Juma ni moja ya mwanamke ambaye alijifungualia njiani kutokana na ukosefu wa zahanati katika kijiji hicho anazeleza juu ya kisa hicho.

Pichani Bi. Fatma Juma ni moja ya mwanamke ambaye alijifungua njiani kutokana na ukosefu wa zahanati katika kijiji hicho.
Sauti ya Bi. Fatma Juma

Kwa upande wake Agida Omary Ford ambaye ni afisa Mipango kutoka halmashauri ya Wilaya ya Chemba anaelezea hatua ambazo watachukua baada ya wananchi hao kuibua changamoto ya ukosefua kituo cha afya.

Pichani Bi. Agida Omary Ford Afisa Mipango halmashauri ya Wilaya ya Chemba
Sauti ya Bi. Agida Omary Ford

Awali Mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la AFNET Joy Njelango ameelezea umuhimu wa jamii kushiriki katika kuibua changamoto zinazowakabili ili ziweze kuweka kwa mpango wa kata kwa ajili ya utekelezaji.

Pichani Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AFNET Joy Njelango
Sauti ya Bi. Joy Njelango

Tangu kijiji hicho kuanzishwa mwaka 1970  hakijawahi kuwa na zahanati hali inayokwenda tofauti na Sera ya Afya ya Juni 2007,ambayo inaeleza kuwa  zahanati inapaswa kuwapo kwenye kila kijiji na kituo cha afya kwa kila kata.

Pichani wananchi waliojitokeza katika mkutano na wa shirika lisilo la kiserikali la AFNET kujadili changamoto ya kukosekana kwa zahanati Peranga Chemba.