Dodoma FM
Mbegu za asili zinavyohimili changamoto mabadiliko tabianchi
12 November 2024, 10:22 am
Na Mindi Joseph.
Licha ya kuwa zipo katika hatari ya kupotea, mbegu za asili zimetajwa kuwa bora katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Afisa uwezeshaji kutoka katika Shirika la Pelamu Anna Malwa amesema mbegu za asili zina virutubisho vingi vinavyosaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi japo zipo hatarini kupotea.
Aidha wakulima wadogo wamesifia uwezo wa mbegu za asili katika kilimo kwa kuwa na mahitaji machache ya huduma kulinganisha mbegu za kisasa.