Je nini husababisha mimba na ndoa za utotoni ?
24 October 2024, 7:48 pm
Na Anwary Shabani
Hali ya umaskini imeendelea kutajwa kuwa moja ya chanzo cha mimba na ndoa za utotoni katika maeneo mbalimbali nchini.
Bwn. Michael Laurent Mavunde kutoka Shirika la Afya Community Care lilipo jijini Dodoma anaeleza sababu mbalimbali zinazotajwa kama chanzo cha tatizo hilo.
Aidha Daudi Tandila kutoka Shirika hilo naye ameeleza athari zinazojitokeza kuhusiana na tatizo hiko.
Kwa upande wa wananchi kutoka maeneo mbalimbali jijini Dodoma wameeleza mambo yanayopelekea kuwa chanzo cha mimba na ndoa za utotoni.
Sanjari na hayoo Michael Mavunde ameshauri nini kifanyike ili kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.
Utafiti wa afya ya uzazi na mtoto Pamoja na viashiria vya malaria Tanzania kwa mwaka 2022 unaonyesha kuwa Tanzania imepunguza mimba za utotoni kwa asilimia tano ndani ya miaka mitano ikiwa ni sawa ana asilimia moja kwa mwaka.