Vitongoji 150 kupata umeme wa REA Dodoma
18 October 2024, 8:04 pm
Na Mariam Matundu.
Vitongoji mia moja na hamsini katika mkoa wa Dodoma vinatarajia kufikishiwa umeme wa REA kupitia mpango wa vijiji kumi na tano kila jimbo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ameyasema hayo Oct. 18, 2024 wakati wa kutambulishwa mkandarasi atakaetekeleza mradi huo kupitia wakala wa nishati vijijini REA . Senyamule amesema kuwa mpango huo utawezesha vitongoji 1781 kati 2892 vinavyohudumiwa na REA kwa mkoa wa Dodoma kufikiwa na huduma ya umeme. Kikao cha kumtambulisha mkandarasi kimefanyika Oct 18, 2024 ofisini kwa Mkuu wa mkoa jijini Dodoma.
Mhandisi Msimamizi wa REA kanda ya kati Anneth Malingumu amesema kuwa mradi huo utagharimu shilingi bilioni 18.5 ambapo kwa mkoa wa Dodoma utatekelezwa kwa miezi 24 .
Vitongoji 1781 kati ya vitongoji 2,892 imekwisha kupatiwa umeme kupitia miradi mbalimbali ya Wakala na Tanesco ambapo vitasalia vitongoji 1111 vitaendelea kupatiwa umeme katika awamu nyingine.