Dodoma FM

Kongamano la 10 la joto ardhi Afrika laja na fursa za kiuchumi

3 October 2024, 8:10 pm

Na Alfred Bulahya

Kongamano la 10 la joto ardhi barani Afrika linatarajia kufanyika mnamo 21-27 Oktoba 2024  katika Kituo cha Mikutano cha JNICC, Dar es Salaam na litaenda sambamba na kaulimbiu isemayo Kuharakisha Maendeleo ya Rasirimali za Joto Ardhi katika Afrika, masoko ya Gesi ya ukaa, na Upunguzaji wa gesi ya ukaa.

.Kongamano hilo ambalo litatawaleta pamoja wadau mbalimbali katika sekta ya nishati duniani , linakuja ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali ya Jamhuri ya Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha asilimia 80 ya wananchi wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2030.

Akiongea na waandishi wa habari hii leo jijini Dodoma Meneja Mkuu wa uendelezaji Joto ardhi Tanzania Mhandisi Mathew Mwangomba ameeleza mambo muhimu yatayofanyika katika kongamano hilo.

Meneja Mkuu wa uendelezaji Joto ardhi Tanzania Mhandisi Mathew Mwangomba
Sauti ya Mhandisi Mathew Mwangomba

Katika hatua nyingine amesema kongamano hilo litatoa fursa kwa washiriki kufanya ziara za kisayansi katika maeneo ya miradi ya joto ardhi iliyopo kwenye mikoa ya Songwe na Mbeya.

Pichani ni waandishi wa habari wakati mkutano na waandishi wa havbari
Sauti ya Mhandisi Mathew Mwangomba
Pichani ni waandishi wa habari wakati mkutano na waandishi wa havbari

Makamu wa Rais, wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la 10 la joto ardhi Barani Afrika.