Dodoma FM

Mtindo wa maisha chanzo magonjwa ya moyo kwa vijana

1 October 2024, 7:53 pm

Vijana kwa sasa wamekuwa waathirika wakubwa wa magonjwa ya moyo Nchini Tanzania ukilinganisha na maeneo mengine Duniani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital wa Benjamin Mkapa Prof Abel Makubi amebainisha hilo wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuelekea kambi maalumu ya magonjwa ya moyo itakayofanyika Hospital hapo kwa kushirikiana na madaktari kutoka uholanzi.

Pichani Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital wa Benjamin Mkapa Prof Abel Makubi
Sauti ya Prof Abel Makubi

Ameongeza kuwa tatizo hilo linakuwa kutokana na vijana kushindwa kubadili mtindo wa Maisha.

Sauti ya Prof. Abel Makubi

Aidha Dkt Grandjea Gerhard kutoka uholanzi amesema kuwa amesema kuwa umuhimu wa nchi ya Tanzania kuwa na kituo kingine cha matibabu ya moyo tofauti na taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete.

Dkt Grandjea Gerhard kutoka Uholanzi
Sauti ya Dkt Grandjea Gerhard

Sambamba na hayo wataalamu kutoka uholanzi wametoa vifaa vya takribani milioni mia nne kwa ajili ya kusaidia wasio na uwezo kutokana na tiba ya moyo kugharimu fedha nyingi.

Pichani washiriki wakati Prof. Abel Mkubi akiongea na waandishi wa habari